Diamond Aweka BIFU Pembeni Aonesha Ukomavu Wake na Kuitangaza Album ya Harmonize Kwenye Page yake | ZamotoHabari.

Msanii wa muziki @diamondplatnumz amepost cover ya albamu mpya ya AfroEast ya muimbaji @harmonize_tz ambaye alikuwa msanii wa label yake ya WCB.

Hatua hiyo imetafsiriwa ni hatua nzuri toka mkali huyo wa wimbo Never Give Up aondoke katika label hiyo ambayo ilimtoka kimuziki.

Harmonize siku ya jana alizindua albamu yake hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.

Katika usiku huo muimbaji huyo aliushukuru uongozi wake huo wa zamani kwa kumvumilia mpaka amefika hatua ya kumalizana nao.

Msanii wa muziki Shilole pamoja na Shetta ni miongoni mwa wasanii waliofurahiachatua hiyo licha ya baadhi ya watu kuwa na mtazamo tofauti huku wengine wakidai ni mtego.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini