Mrembo Haitham Kim amefunguka na kusema Amber Lulu ni mshamba na hana hadhi ya kutembea na mwanaume wake kwa sababu haendani naye.
Haitham Kim amesema hivyo baada ya kuwepo na stori zinazoelezwa kuwa Amber Lulu amemuibia mwanaume wake aitwaye Boshen, kisha kujirekodi wote video na kupost katika mtandao wa Instagram.
"Amber Lulu hawezi kunichukulia mwanaume wangu hana hiyo hadhi, ukimuangalia mpenzi wangu Boshen na Amber ni vitu viwili tofauti, aliamua kufanya ushamba tu wa kujirekodi video na kupost instagram na kuandika vitu anavyovijua yeye na sipendi kumuongelea maana nitampa kiki" amesema Haitham Kim.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments