Harmonize Feki Achezea Kichapo Kisa Mwanamke Aliyemtongoza DM | ZamotoHabari.


Moja kati ya video inayozunguka kwa sasa mitandaoni, inamuonesha jamaa mmoja akichezea kichapo kutoka kwa mwanamke aliyemdanganya kuwa yeye ni Harmonize wakati sio kweli ili mradi awe naye kwenye mahusiano.


Jamaa huyo ambaye jina lake halijajulikana, amechezea kichapo hicho mbele ya waandishi wa habari huku mwanamke huyo akiwa amemkunja shingoni, huku akimuuliza kwanini amemdanganya kuwa yeye ni Harmonize katika mtandao wa Instgram.

Katika utetezi wa jamaa huyo alisikika akisema "Muonekano ni kama hivi unavyouona ni fresh tu, mimi nafanana na Harmonize sijifananishi bali nafananishwa na watu ausio ila nampenda sana".

Aidha wakati huo mwanamke huyo alikuwa anampiga kichwani huku amemkunja na kumuuliza  "Kwanza usiniguse wewe una Corona, ongea vizuri kwanini umeamua kunidanganya wewe ni Harmonize na ukanitongoza Instagram".


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini