JESHI LA MAGEREZA LA SITISHA KUTEMBELEWA KWA WAFUNGWA NA MAHABUSU GEREZANI, MAHABUSU WAPYA KUPOKELEWA KWA KUHAKIKI AFYA ZAO | ZamotoHabari.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
MAHABUSU wapya kupokelewa Gerezani mara baada ya kufanyiwa vipimo vya afya zao hii ni kufuatia kwa kuripotiwa kwa uwepo wa ugonjwa wa Corona (Covid-19) nchini.

Akizungumza na MICHUZI BLOG, Msemaji wa jeshi la magereza SSP. Amina Kavirondo amesema kuwa baada ya kupimwa mahabusu wapya na kujiridhisha kuwa wako salama kwa maana hata polisi nao watakuwa wamechukuwa hatua kwa mahabusu hao.

"Na sisi watakapofika kwenye himaya ya kwetu tutachukua hatua ya kuhakikisha usalama wa afya zao huku tukisubiri miongozo mingine ya serikali." Amesema SSP. Amina

Hii ni kutokana na Jeshi la magereza kusitisha  kutembelea wafungwa na mahabusu gerezani kuanzia Machi 18,2020. Ikiwa ni pamoja na kusitisha kupelekewa chakula kwa mahabusu waliopo gerezani.

Akizungumza kuhusiana na sehemu ambapo watawekwa kwa siku 14 SSP. Amina amesema "Kutakuwa na utenganisho wa muda na baadae utafanyika utaratibu wa wa kuwahifadhi kama walivyo mahabausu wengine na utenganisho utamuhusu yule ambaye atahisiwa lakini iwapo atathibitika yuko sama ataendelea na maisha yake gerezani kama walivyo wengine."

Hata hivyo SSP. Amina ametoa rai kwa yeyote ambaye ataonekana na dalili asipelekwe eneo la gerezani ingawa jeshi la magereza na jeshi la polisi wanawasiliana.



Jeshi la litaendelea kuchukua kila tahadhali na hatua kwa kadri litakvyoona inafaa sambamba na kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali dhidi ya janga la ugonjwa wa Corona.




APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini