KIMENUKA..Marekani na China Zatupiana Lawama Juu ya Corona...Trump Ajibu Kwanini Anaviita Virusi vya China | ZamotoHabari.



Vita vya maneno vinaendelea kati ya Marekani na China, ambapo nchi hizo zinatupiana lawama kuhusu janga la #Coronavirus baada ya China kumshtumu Rais Donald Trump wa Marekani kwa kujaribu kuilaumu China kuhusu janga hilo

Machi 19, 2020 Trump alisema kuwa dunia inalipa deni kubwa kutokana na ukosefu wa uwazi wa China wakati mlipuko wa #Coronavirus ulipozuka katika mji wa Wuhan mwishoni mwa mwaka jana

China imekosolewa vikali kwa kuficha ukweli kuhusu virusi hivyo na hata kuwaadhibu baadhi ya watu waliofichua siri kuhusu virusi hivyo mwanzo kabisa vilipotokea

Kwa mujibu wa data za shirika la habari la AFP, ugonjwa wa #COVID19 umewaua karibu watu 10,000 huku wengine 232,000 wakiambukizwa duniani kote

Katika moja ya Press Conference , Mwandishi mmoja wa habari amemuuliza Trump kwanini unaita Corona Chinese Virus, Trump akajibu kwa kifupi tu kuwa kwasababu vimetoka china

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini