Marry "Anayedanga Anipigie Simu Mimi Nimpe Pesa" | ZamotoHabari.


Muigizaji  wa filamu hapa nchini Marry Blizzy amefunguka kusema  wanawake wote ambao wanatabia ya kudanga wampigie  simu yeye kisha atawapa pesa ili mradi waache kudanga kwa sababu wanatumika sana.


Akizungumza na eNewz ya East Africa TV inayoruka siku ya Jumatau hadi Ijumaa kuanzia 12:00 jioni mpaka 12:30, Marry Blizzy amesema wanawake wenye tabia hiyo hawawezi kuwa watamu kwa sababu wanaweza kutumika na wanaume watano kwa usiku mmoja ili wapate pesa.

"Ukiona mtu nipo naye kwenye mahusiano jua nina hisia naye, na  mapenzi ndiyo yamenipeleka kwake sio kudanga, ila  kwa wanawake ambao wanadanga kwa ajili ya Elfu 20, 50  au hata Laki 1 wanipigie simu niwape hiyo pesa waache kudanga, kwa sababu hizo pesa ni ndogo  itawasaidia nini, halafu watadanga kwa wanaume wangapi" ameeleza Marry Blizzy


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini