X-Ray ya Mdee alivyovunjika mkono, Bulaya aumia mgongo na kifua baada ya kutembezewa kichapo | ZamotoHabari.



X-ray ya mkono wa mbunge wa Kawe (Chadema),Halima Mdee, inayoonyesha jinsi alivyovunjika mkono baada ya kutembezewa kichapo juzi  walivyokwenda kumpokea Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitoka gerezani.

Mdee pamoja na Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya wamelazwa katika hospitali ya Agakhan baada ya kutembezewa kichapo na askari magereza wa gereza la Segerea.


 Mbunge wa Tarime vijijini (Chadema), John Heche, amesema amewatembelea Mdee, Bulaya na Jesca Kishoa hospitali bado wapo kwenye maumivu makubwa.

“Halima amevunjwa mkono wa kulia, mh Bulaya ameumia mgongo na kifua,” aliandika Heche katika ukurasa wake wa Twitter.

Alisema anaamini walichosema magereza ni uongo kama wanajiamini watoe picha za CCTV.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini