Mtu wa kwanza ajitolea kufanyiwa chanjo ya virusi vya corona Marekani | ZamotoHabari.

Binadamu wa kwanza kufanyiwa jaribio ya chanjo ya kinga dhidi ya virusi vya corona ameanza kufanyiwa jaribio hilo nchini Marekani.

Wagonjwa wanne walidungwa sindano ya virusi katika kituo cha utafiti Kaiser Permanente mjini Seattle, Washington, limeripoti shirika la habari la Associated Press.

Chanjo hiyo haiwezi kusababisha Covid-19 lakini ina jeni la virusi ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa.

Wataalamu wanasema itachukua miezi mingi kujua ikiwa chanjo hii, au utafiti mwingine, utafanikiwa.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini