Viwanja vya ndege Marekani vyashuhudia wimbi la misururu mirefu ya ukaguzi | ZamotoHabari.

Ghasia zimeshuhudiwa katika viwanja vya ndege vya Marekani wakati ambapo hatua mpya za ukaguzi kwa sababu ya virusi cha Corona zinaanza kutekelezwa dhidi ya watu wanaorejea nchini humo kutoka Ulaya.

Kumekuwa na foleni ndefu huku wasafiri wakisubiri kwa saa kadhaa kukaguliwa kabla ya kupita kwenye ofisi za forodha.

Awali, Makamu Rais wa Marekani Mike Pence amesema kuwa Uingereza na Ireland Jumanne zitaongezwa kwenye orodha ya nchi zilizopigwa marufuku kuingia nchini humo pamoja nchi zingine za Ulaya zilizotambuliwa.

Marekani ina visa zaidi ya 2,700 vya corona huku vifo 54 vikiwa tayari vimethibitishwa.

Wachambuzi wanasema kwamba, kwa sasa hali ya taharuki imetanda nchini Marekani huku kukiwa na hofu ya huduma za hospitali kutoweza kufikia wote wenye hitaji la haraka pamoja na huduma kwa watoto wakati ambapo mamilioni ya wanafunzi wanarejea nyumbani.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini