SAMIA NA JAKAYA WAUNGANA NA WADAU KUCHANGIA HARAMBEE YA UJENZI WA UKUMBI WA CCM PWANI | ZamotoHabari.

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MAKAMU wa Rais na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu pamoja na Rais mstaafu Jakaya Kikwete  wameungana na wadau , kwenye harambee ya kuchangia zaidi ya sh.milioni 500 ili kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa CCM mkoani Pwani,":ambapo ameeleza chama hicho mkoa sio maskini badala yake waviendeleze vitega uchumi walivyonavyo.

Katika harambee hiyo, imeweza kupatikana kiasi cha sh.milioni 584.1 ikiwa fedha taslim milioni 113.4,ahadi milioni 471.6,mifuko ya saruji 400 na ndoo za rangi 50.

Akizungumza katika harambee hiyo iliyofanyika mjini Kibaha,Samia alieleza alisema ofisi yake inachangia milioni kumi na kudai ,jengo hilo lilisuasua kwa kipindi kirefu lakini chini ya usimamizi wake atasimamia ujenzi huo na hakuna fedha wala nondo zitakazopotea kama zilivyopotea wakati huo.

Alisema, CCM Pwani ina vitega uchumi ,lakini waache kubakia kuvihesabu kwa namba ,wasilale badala yake waviendeleze ili kupiga hatua kiuchumi na kuondokana na hali ya kuwa omba omba.

"Sisi sio masikini wa namna hiyo, tuliendekeza matumbo kuliko lililo mbele yetu, sasa tuache kuendekeza matumbo tufanye kazi,mkoa wa Pwani hauna sababu ya kupita kuombaomba, maana mna mtaji lakini pia mmelala"

"Tujipange vizuri, itabakia tunasema hiki chetu,kile chetu lakini hamviendelezi"alibainisha Samia.

Samia alifafanua, wahakikishe jengo hilo linakamilika mwezi June mwaka huu ili kuondokana na kupanga ukumbi wakati wa shughuli za chama.

Nae ,Jakaya Kikwete alishukuru na kufurahi kwa kualikwa kwenye shughuli hiyo,na atachangia mifuko 200 ya saruji.

Jakaya alisema ,wazo la ujenzi huo lina historia kwake, lilianza miaka mingi ,":Nimefurahi sana kuona msukumo wa kuendeleza vitega uchumi hivi ambavyo vilisuasua lakini sasa vinaendelezwa kwa manufaa ya chama."alisema Jakaya.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo  ,aliwaomba ,wadau na wananchi kuendelea kuchangia ili kutimiza adhma hiyo.

"Tumepewa muda ,hadi mwezi June mwaka huu ,ujenzi uwe umekamilika hivyo juhudi za pamoja zinatakiwa ili tukamilishe kwa wakati huo"alifafanua Ndikilo.

Katika harambee hiyo, mfanyabiashara Bakhresa amechangia kiasi cha sh.milioni 100,Shubash Patel anaezeka jengo zima kwa gharama ya milioni 250.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Ndikilo alitoa sh.milioni 50,kamati ya siasa mkoa mifuko 200 ya saruji na sh.milioni nne,wabunge 13 wa mkoa huo wamechangia sh.milioni 16,ambapo rafiki wa mbunge wa viti maalum Zainab Vullu amechangia milioni 10.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini