Umoja wa Mataifa wapongeza kuundwa baraza la mawaziri Sudan Kusini | ZamotoHabari.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza hatua ya kuundwa baraza la mawaziri la serikali ya mpito ya umoja wa kitafa nchini Sudan Kusini.

Kwenye taarifa yake msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephanie Dujaric, amesema Guterres amepongeza moyo wa maelewano na ushirikiano uliooneshwa na pande husika, ambao umeleta maendeleo haya muhimu.

Guterres amesisitiza utayari wa Umoja wa Mataifa kusaidia pande za Sudan Kusini kutekeleza makubaliano ya Amani ya mwaka 2018, kwa kushirikiana kwa karibu na Shirika la Maendeleo ya Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki IGAD pamoja na Umoja wa Afrika.

Siku ya Alhamisi rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alitangaza majina ya mawaziri wapya watakaounda serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo.

Kwa jumla, serikali hiyo itaundwa na mawaziri 34 na manaibu waziri 10.

Vita vya ndani nchini humo vilivyoanza Disemba 2013 vimesababisha mauaji ya maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. Nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya ndani baada ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar wa kabila la Nuer kwamba alihusika na jaribio la kupindua serikali yake.

Nchi ya Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011 kwa uchochezi wa nchi za Magharibi hususan Marekani. 
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini