Walioambukizwa kirusi cha corona Afrika Kusini wafikia 38 | ZamotoHabari.


Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imetangaza kuwa, idadi ya watu walioambukizwa kirusi hatari cha corona nchini humo jana ilipanda hadi watu 38 kutoka 24 waliokuwa wameambukizwa kirusi hicho hadi juzi Ijumaa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu 14 waliokumbwa na ugonjwa wa COVID-19 wameongezeka katika kipindi cha siku moja nchini Afrika Kusini.

Huku hayo yakiripotiwa, idadi ya walioambukizwa kirusi cha corona imeongezeka mara mbili pia nchini Morocco baada ya nchi hiyo kuripoti kesi nyingine 9 za maambukizi ya kirusi hicho jana Jumamosi. Hadi kufikia jana, watu 17 walikuwa wameshaambukizwa corona nchini humo kwa mujibu wa wizara ya afya ya Morocco.

Kati ya kesi hizo mpya za maambukizi ya kirusi cha corona, imo moja ya mtu wa ndani ya Morocco kwenyewe wakati kesi zilizobakia ni za watu waliotoka katika nchi za Ulaya za Uhispania, Italia na Ufaransa.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini