WAFANYABIASHARA 10 WA MADUKA MJINI MOSHI WALAZIMIKA KUVUNJA MAKUFULI BAADA YA KUFUNGIWA MADUKA YAO NA MGAMBO WA MANISPAA YA JIJI | ZamotoHabari.

 
 
 
Na Woinde Shizza,KILIMANJARO

Wafanyabiashara kumi  wanao miliki maduka katika Eneo la stendi kubwa Moshi Mkoani Kilimanjaro wamelazimika kuvunja kufuli Mara baada ya kufungiwa maduka yao   na mgambo wa Manispaa kwa madai kwamba sio wapangaji halali 

Wakizungumzia tukio hilo kwa niaba ya wafanya biashara hao Iren Charles ameleza kwamba wananyanyasika na Mgambo wa Manispaa ya Moshi kwa  kuwavamia na kufunga maduka yao hivyo kukazimika kuvunja kufuli hizo.

Ameeleza kuwa  walifungua kesi Mahakamani ya kupinga kufungiwa maduka yao  na mahakama kuwaruhusu kuendelea na Biashara kama kawaida lakini mgambo wamekua wakifika katika maduka yao na kulazimisha kufunga kwa nguvu .

Ameongeza kuwa wao wamemiliki maduka hayo kwa muda mrefu zaidi ya miaka 15  huku wakilipa kodi zote na kutambulika na manispaa ya Moshi lakini sasa kilichotokea ni madalali kuingilia kukodisha maduka yao kwa garama kubwa sana.

Amesema kwamba madalali ndio chanzo cha wao kukosa maduka hayo kwani tenda ilio tangazwa ilikua ni kubwa yenye lengo la kuwakwamisha kibiashara kwa  kuwataka kulipa kiasi cha shilingi laki tatu kwa mwezi jambo ambalo wamedai hawawezi kulipa gharama hiyo 

Wafanya biashara hao wameomba viongozi wa serikali kuingilia kati kwani wananyanyasika kufungiwa maduka yao huku wao ni wazawa wanaitaji kulipa Kodi na kuleta maendeleo katika manispaa yao 

Akijibu swala Hilo   Mkurugenzi wa mansipaa ya Moshi Maiko Mwandezi anasema ni kweli walikua na mikataba na wafanyabiashara hao lakini ilisha Kwisha na walitangaza tenda kwa mujibu wa sheria na tends ilivyo pita awakushinda na kutakiwa kukabidhi maduka hayo 

Amesema kwamba  wafanyabiashara wanacho kifanya ni kuleta vurugu tu kwani mpaka sasa wamesha vunja makofuli zaidi ya 70 katika maduka walioweka zuio la kutoingia na kutaka kukabidhi maduka kwa walioshinda tenda ambao ni wapangaji wapya 

Kuhusu kutambua zuiyo lilotolewa na Mahakamani mkurugenzi amesema kwamba wanalitambua na wafanya Biashara walipaswa kufunga maduka mpaka hapo kesi ya msingi itakapo kwisha Mahakamani lakini wameendelea kufanya biashara bila kua na mikataba jambo ambalo ni kinyume na sheria 

Hata ivyo mkurugenzi amedai kuwaburuza Mahakamani wafanya biashara hao wapatao 10 kwani kati ya wafanya biashara wapatao 130 hao 10 ndio wanao sumbua serikali kwa kuikosesha mapato kwa muda wote walio pewa barua za kuondoka na kuachia maduka hayo  .

 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini