WAMILIKI WA MAGARI YA MASAFA MAREFU ARUSHA WAUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA VIRUSI VYA CORONA | ZamotoHabari.


Na Woinde Shizza,Arusha

CHAMA cha Wamiliki wa magari ya masafa marefu  Mkoa wa Arusha ,TABOA,Hakiboa pamoja na wasafirishaji wenza  wameiunga mkono serikali katika swala la kupiga vita ugonjwa wa Corona pamoja na kutoa elimu ya kuchukuwa taadhari kuhusu ugonjwa huo.

Ambapo wameamua kunua dawa ,mabomba ya kunyunyuzia dawa ,dawa za kunaiya mikono na ndoo 100 za kuwia mikono huku wakizindua rasmi mchakato wa  upigaji dawa kwa vyombo vyote vya usafirishaji  vilivyopo mkoani hapa.

Akizungumza wakati wa kukabithi vifaa hivyo leo Machi 27,mwaka 2020, Katibu wa TABoa ambaye pia ni mmiliki wa mabasi ya abiria ya Kimotco Benedict  John Mberesero (Ben Kimotco)  amesema  wameamua kuunga mkono juhudi za  serikali katika suala zima la kupiga vita Corona kwani  ni ugonjwa unaorikisa dunia nzima kwa sasa kwa kununua vifaa ambavyo vinaweza kuwakinga wananachi juu ya ugonjwa huu .

 Amesema kuwa vifaa hivyo walivyonunua vinagarimu kiasi cha shilingi milioni 13  na watavisambaza katika maeneo yote ya mkoa wa Arusha ambapo alaibainisha pia watahakikisha vyombo vyote vya usafiri vinapigwa dawa kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huo.

Ameongeza  kuwa mchakato huo  umeeanza ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha na wanatarajia kulifanya katika halmashauri zote za mkoa wa Arusha .

“Hatutakubali kuona mtu anakufa kutokana na ugonjwa huu kitu tutakacho kifanya tutatoa elimu kwa abiria wetu ,wananchi wote wanaoingia standi na kupanda magari yetu juu ya kuchukuwa taadhari ya ugonjwa huu ,na nisema tu swala hili tunaomba tuwaambie abiria wasikatae kunawa mikono pale tunapo waambia wanawe ,kwani wakifanya hivyo watakuwa wanavunja sheria na iwapo mtu akivunja sheria tutamchukulia hatua kali maana atakuwa atutakii mema ,“amesema Benedict

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewapongeza viongozi hao kwa kuunga mkono Serikali katika kupiga vita ugonjwa huo na kubainisha Corona ni mbaya,  hivyo ni vyema kila mwananchi kuchukuwa taathari.

 Aiidha amewataka wananchi kufuata maagizo yote ambayo  wanapewa na viaongozi wa afya juu ya njia za kujikinga na ugonjwa huo.
 
Pia amesema wananchi wanatakiwa  kuondoa taaruki na kutotishana  bali waendelee kuchukuwa taathari huku akiwasihi  kila mwananchi kuchukuwa tahadhari katika eneo lake na kuendelea kusikiliza miongozo inayotolewa na wataalam wa afya.

“Kuna tabia imezuka ya watu wenye maduka wanaouza sanitizer kupandisha bei, napenda niwaambie wananchi kile kidogo kinauzwa elfu tatu ukienda maahali ukakuta kinauzwa zaidi nipigie simu ,naniwaambie wauzaji  msipandishe bei  tukibaini mmepandisha bei hatu kali zakisheria tutawachukulia ,naniwasisitize wananchi tuzingatie usafi ugonjwa huu ni mbaya na unaua hivyo tujitaidi sana kuwa wasafi ili ugonjwa huu usitumalize, "amebainisha Gabriel

Wakati huo huo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi  Almachius  Muchunguzi amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kutii sheria bila shuruti ili kuepuka kuambukizwa ugonjwa huu ,

‘’Iwapo umeambiwa usibebe abiria zaidi ya ukabeba  apo utakuwa unavunja sheria na sisi kama jeshi la polisi atutakuvumilia,tukikwambia msikae kwenye mikusanyiko tukikukuta atutakuvumilia kwakweli hatua kali tutakuchukulia ,tukikwambia kaandani ukatoka utakuwa unavunja sheria na sisi atutakuvumilia ,ukileta maneno ya kizushi hatuta kuvumilia hivyo ni wasihi tu wananchi wa mkoa wa Arusha mtii sheria bila shuruti ili tuweze kujikinga na ugonjwa huu “amesema.

 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akipuliza dawa ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona katika moja ya mabasi kwenye uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika stendi ya mabasi makubwa jijini humo.
  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akipuliza dawa ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona kwenye moja ya Kofia ngumu ya Dereva wa Boda boda katika moja ya kituo cha Waendesha Boda boda na Kituo cha mabasi kwenye uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika stendi ya mabasi makubwa jijini humo.
 Katibu wa Taboa mkoa wa Arusha Benedict John Mberesero akiongea katika zoezi la kupiga dawa mabasi yaendayo masafa marefu Jana, ambapo alisema kuwa wao kama wamiliki wa mabasi  wameunga mkono Serikali katika swala zima la kupiga Vita gonjwa hili la corona ambapo wameweza kutoa ndoo za kwaajili ya kuweka standi 100,vinyunyizi 6 pamoja na dawa zenye thamani ya shilingi milioni 13 ,pia amesema mtu yoyote ambaye hatafuata masharti apigwe viboko (picha na Woinde Shizza,Arusha)



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini