WANANCHI TANDAHIMBA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA UGONJWA WA CORONA | ZamotoHabari.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Benaya Kapinga amewataka  wananchi kuchukua tahadhari na ugonjwa wa corona kwani Wilaya hii ipo mpakani

Akizungumza leo Wilayani hapa  Kapinga amesema kuwa wananchi  wanatakiwa kuacha kusalimiana kwa kushikana mikono ili kujikinga na Corona

Amesema kila mwananchi ahakikishe ana nawa mikono na maji tiririka  na sabuni ikiwa ni miongoni mwa hatua za awali za kujikinga

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Antpas Swai amesema tayari  wametenga Zahanati ya mtegu kwa ajili ya wagonjwa watakaopatikana na corona ndani ya Wilaya hiyo

Sambamba na Hilo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela amesema wanatarajia kuagiza  vipima joto mwili ambavyo vitasaidia kupima joto kwa mbali hususan kwenye maeneo ya mpakani
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Benaya Kapinga
 Unaweza kuitumia picha hii ya Kaimu DC Benaya Kapinga akiwa na afisa Afya
 Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antpasi Swai
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela akielezea jambo


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini