Anthony Joshua "Baadhi ya Watu Waliniita ‘Mwendawazimu’ kwa Kukubali Kurudiana na Andy Ruiz Jr" | ZamotoHabari.


Bingwa wa ngumi uzito wa juu duniani, Anthony Joshua, amesema aliitwa ‘Mwendawazimu’ na baadhi ya watu, kwa kukubali kwake kucheza pambano la marudiano na Andy Ruiz Jr, miezi michache tu baada ya kupoteza dhidi ya Mmexico huyo.


Joshua alifanikiwa kurejesha mikanda yake ya ubingwa wa uzito wa juu ya IBF, WBA na WBO kutoka kwa Ruiz Jr mwezi in Disemba, miezi sita baada ya kuipoteza.

AJ amesema kuwa aliamua kutosikiliza ushauri wa watu, waliomchukulia kama mwendawazimu kwa hatua yake ya maamuzi ya kukubali kurudi ulingoni kwaajili ya pambano la marudiano.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini