Virusi vya corona: Waziri Mkuu Boris Johnson apelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi | ZamotoHabari.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepelekwa katika chumba cha kuhudumia wagonjwa mahututi baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya kwa siku kumi zaidi kwasababu ya ugonjwa wa virusi vya Corona, kwa mujibu wa msemaji katika makazi ya Waziri Mkuu.

Bwana Johnson amemuambia Waziri wa mambo ya nje Dominic Raab kuchukua usukani "pale ambapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo", msemaji ameongeza.

Waziri Boris ,mwenye umri wa miaka 55, alilazwa katika hospitali ya St Thomas mjini London wakati hali yake ya kiafya ilipokuwa haina ahueni huku homa na kukohoa kukiongezeka zaidi siku ya Jumapili. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya ushauri kutoka kwa timu yake ya matibabu na anaendelea kupata huduma stahiki.

Taarifa zaidi zinaarifu kuwa : "Tangu Jumapili jioni, Waziri huyo Mkuu amekuwa chini ya madaktari wa hospitali ya St Thomas mjini London, baada ya kuonesha dalili mbaya za virusi vya Corona.

"Mchana wa leo, hali ya Waziri Mkuu hali ya afya yake imezidi kuzorota na kutokana na ushauri uliotolewa na timu yake ya madaktari, amehamishwa hadi kitengo cha wagonjwa mahututi hospitalini humo."

Mapema Jumatatu ujumbe uliandikwa kwenye mtandao wa Twitter ukiashiria kwamba anaendelea kupata afueni.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini