Fatma Karume: Ukiona mabeberu wana hofu kubwa na Corona, tujitahidi kuchukua tahadhari | ZamotoHabari.


Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume,  amesema amesoma barua iliyokwenda kwa Raisa John Magufuli kuhusu Covid-19 na ushauri kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).

“Jamani ninakuombeni tena na tena kama mnaweza kaeni majumbani na epukeni mikusanyiko,” aliandika Fatma katika ukurasa wake wa Twitter.

“Ukiona mabeberu wamepanic hii kitu ikitupata wengi itakuwa balaa nimesoma yanayotokea ECUADOR yana huzunisha,”

Aliandika ujumbe huu “Nimeisoma hiyo barua kwenda kwa Magufuli kuhusu Covid-19 na ushauri wa WHO. Jamani ninakuombeni tena na tena, kama mnaweza kaeni majumbani na epukeni na mikusanyiko. Ukiona mabeberu wamepanic hii kitu ikitupata wengi itakuwa balaa imesoma yanayotokea ECUADOR yana huzunisha,”


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini