Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema Mungu amsaidie Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy mwalimu asije kupotosha taarifa.
“Hali ikiwa mbaya watu wakafa wanao kutuma kama wapo watakuruka,” aliandika Lema katika ukurasa wake wa Twitter.
Lema alisema anashukuru Mungu kwa idadi ndogo ya wagonjwa nchini.
“Lakini sijui ni kwa nini akili yangu ina mgogoro na takwimu zako? Nitaongea na akili yangu tens Leo kabla sijalala,” aliandika Lema
Waziri Ummy,Mungu akusaidie usije kupotosha taarifa.Hali ikiwa mbaya watu wakafa wanao kutuma kama wapo watakuruka,namshukuru Mungu kwa idadi ndogo ya wagonjwa Nchini.Lakini sijui ni kwanini akili yangu ina mgogoro na takwimu zako?nitaongea na akili yangu tena leo kabla sijalala— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) April 3, 2020
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments