GAVANA APINGWA JUU YA MPANGO WAKE WA KUTUMIA POMBE KAMA KITAKASA KOO | ZamotoHabari.


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

LICHA ya Shirika la Afya Duniani kusema wazi kuwa pombe haiwezi kupigana dhidi ya virusi vya Corona (Covid-19) na kuwashauri watu wapunguze matumizi yake Gavana wa Mji mkuu wa Nairobi, nchini Kenya Mike Sonko kupitia mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mapema jumanne valithibitisha matumizi ya pombe katika Kupambana na virusi hivyo kwa kile alichoeleza kuwa pombe aina ya Hennessy ni kitakasa koo "throat sanitizer." CNN imeripoti.

Sonko aliwasilisha mpango huo mbele ya waandishi wa habari na kutangaza azma yake ya kuambatanisha chupa ndogo za pombe aina ya Hennessy katika vifurushi vya chakula vitakavyotolewa kwa familia duni wakati wa kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya Corona.

Imeelezwa kuwa Gavana huyo alihalalisha kuingizwa kwa pombe katika vifurushi vya kujikinga na kuenea kwa virusi hiyo ikiwa kama kitakasa koo.

"Nadhani kutokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni na mashirika anuwai, inaaminika kwamba pombe inachukua jukumu kubwa katika kuua virusi vya Corona." Sonko alieleza kwenye video.

"Tutakuwa na chupa ndogo za Hennessy kwenye pakiti za chakula ambazo tutakuwa tukiwapa watu wetu ..." Alieleza Gavana huyo wa Nairobi Mike Sonko.

Ikumbukwe kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonya kwamba kunywa pombe si kinga dhidi ya COVID-19 na inaweza kuwa hatari zaidi na likaweka wazi kuwa pombe hailindi dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona, na kuwashauri watu kupunguza matumizi yake.

Katika chapisho lililotolewa na shirika la Afya duniani (WHO) siku ya Jumanne lilisema kwamba pombe inaweza kudhoofisha afya ya mtu na kufanya wawe katika hatari kubwa ya virusi ikiwa ni pamoja na Covid-19.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Amref Health Africa Githinji Gitahi  ameeleza kuwa pombe ni faida isiyo ya faida ya matibabu, katika chapisho lake kupitia ukurasa wa Twitter alilaani madai ya Sonko na aliwataka Wakenya waondoe pombe hiyo.

Hii sio mara ya kwanza Sonko kukutana na uchunguzi wa madai, Gavana huyo alikamatwa mwishoni mwa mwaka jana kwa tuhuma za ufisadi ambazo alizikana na kulazimika kukabidhi majukumu yake kadhaa kwa serikali ya kitaifa.

Wakati huo huo, kampuni ya vinywaji ya Hennessy  kupitia vyombo vya habari imepinga madai ya Gavana huyo ya kwamba kunywa au kutumia pombe  kunaweza kuzuia virusi vya Corona.

"Hennessy inapenda kusisitiza kwamba unywaji wa chapa yetu au kileo kingine chochote cha pombe hailindi dhidi ya virusi," ilieleza  sehemu ya taarifa yake kupitia News News ya Nairobi.

Imeelezwa kuwa CNN haikuweza kufikia Sonko kwa maoni.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini