Kiwanda cha Sukari kujengwa Kasulu-TIC | ZamotoHabari.


Na Ripota wetu, Kasulu.

Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imetenga eneo la uwekezaji lenye ukubwa wa hekta 35,000 kwa ajili ya kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.

Eneo hilo kwa sasa amepewa mwekezaji wa kampuni ya Kigoma Sugar Co. Ltd chini ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambacho kina mamlaka ya kusimamia Uwekezaji nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange (aliyevaa Fulana rangi ya damu ya Mzee)akifafanua jambo katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe (aliyevaa shati la bluu) na ujumbe wake kutoka katika kituo hicho walipowasili Mkoani Kigoma kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya Uwekezaji Mkoani humo.

Mwekezaji wa Kampuni ya Kigoma Sukari anatarajia kuendesha shamba hilo kwa kulima miwa na kujenga kiwanda cha sukari mapema mwaka huu kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha tani 110,000 za Sukari kwa mwaka, hatua itakayosaidia kupunguza pengo la upatikanaji wa bidhaa hiyo nchini linalokadiriwa kufikia tani 320,000 kwa mwaka.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe (Mwenye shati rangi ya bluu) na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange (mwenye fulana rangi ya damu ya mzee) wakisisitiza jambo wakati wakiangalia ramani ya eneo lililotengwa na wanavijiji wa vijiji saba vya Wilaya ya Kasulu kwa ajili ya uwekezaji, wengine ni maafisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Katibu Tawala wa Mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange alisema eneo hilo limetolewa na Wanavijiji wa Vijini saba vya Nyamidaho, Kumtundu, Nyarugusu, Heru ushingo, Kigadye, Kitanga na Kiyugwe vyote vikipatikana kwenye Kata tatu za Nyamidaho, Kitanga na Heru ushingo, vikiunganisha shamba hilo kuwa moja Wilayani Kasulu Mkoa wa Kigoma.

Mkuu huyo wa Wilaya alikuwa akitoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe, aliyefanya ziara ya kikazi mkoani Kigoma kwa ajili ya kukagua Maendeleo ya Uwekezaji mkoani humo.


Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Simon Anange akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Geoffrey Mwambe (hayupo pichani) aliewasili Wilayani humo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya Uwekezaji.

"Baadhi ya Vijiji kwa hiyari yao wameamua kutoa maeneo ya Uwekezaji, hii ni hatua muhimu na ya kupongezwa sana, shamba hili lenye ukubwa wa hekta zaidi ya a elf 35 linapitiwa na miundombinu yote muhimu kwa Uwekezaji ikiwepo barabara, reli itakayounganisha nchi za Tanzania na Burundi, umeme wa gridi ya Taifa kutoka Nyakanazi hadi Kidahwe Mkoani Kigoma unaotarajiwa kujengwa ifikapo mwakani, pamoja na mto Malagalasi utakaotumika kumwagilia mashamba ya miwa"alisema Kanali Anange.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange (aliyevaa Fulana rangi ya damu ya Mzee)akimwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe (aliyevaa shati la bluu) eneo la shamba la Uwekezaji ilayani humo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe alisema hatua iliyofikiwa na wanavijiji hao ni ya kupongezwa na kwamba (TIC) inaunga mkono juhudi hizo.

"Sisi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) tunaunga mkono juhudi za wanavijiji hawa na tunawapongeza sana,nawahakikishia tutalisimamia eneo hili na Uwekezaji utakaofanywa hapa utakuwa wa manufaa kwa wananchi kwa kuwa nia ya Serikali ni kuifanya Kasulu kuwa kitovu cha uzalishaji wa sukari kwa Mkoa wa Kigoma"alisema Bw. Mwambe.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akiangalia mto Malagalasi unaopita kwenye shamba la uwekezaji Wilayani humo, mto huo utatumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa Sukari.

Kiwanda cha sukari Kigoma  kitakachojengwa kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 110,000 za sukari ambazo zikiingia sokoni zitapunguza pengo la upatikanaji wa Sukari nchini.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini