Leandra Gabriel, Michuzi TV
MWAKA 1665 kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Tauni uliojulikana zaidi kama "Black Death" nchini Uingereza hali iliyopelekea shule, vyuo na huduma mbalimbali za kijamii kuzuiliwa kwa muda kwa lengo la kupunguza kasi ya maambukizi ya Tauni kama inavyofanyika sasa ambapo dunia inakabiliwa na mlipuko wa virusi vya Corona (Covid-19.)
Wakati huo Isaac Newton alikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cambridge na hakuwa Profesa na alilazimika kurudi nyumbani kati ya mwaka 1665 na 1666 baada ya Cambridge kufungwa kutokana na janga hilo.
Newton alirejea Cambridge 1667 na nadharia zinazodumu hadi sasa hiyo ni baada ya kutumia vyema muda huo ambapo janga hilo lilitokea.
Wakati huo wa janga la Tauni "Babonic Plague", Newton akiwa nyumbani alishuhudia tufaa likianguka toka mtini kwenye bustani ya familia huko Woolsthorpe (maili 50 kutoka Cambridge). Hapo alijiuliza maswali yaliyopelekea ugunduzi wa nadharia ya nguvu ya uvutano(Gravity).
Newton alifanya majaribio kadhaa ya mwanga ambayo pia yaliyopelekea kugundua nadharia ya Optiki.Vilevile Newton aliandaa njia na kanuni mpya katika fani ya hisabati na zikawa chimbuko la Calculus.
Janga hilo lilipelekea robo ya wakazi wa Uingereza kufariki kutokana na tauni iliyopiga kati ya miaka ya 1665 na 1666.
Newton alirudi chuoni Cambridge mwaka 1667, akiwa na nadharia alizoziandaa akiwa nyumbani, ndani ya miezi 6 tu alifanywa kuwa mtafiti na miaka miwili alitunukiwa shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Cambridge.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments