Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara wa mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara ndogo ndogo wa matunda na nyanya kando ya mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akionesha mfano wa namna bora ya kunawa wa Mikono kabla ya kuanza ukaguzi wa Kituo cha Afya Kishapu kitachotumika kuhudumia wagonjwa Corana kama atatokea mgonjwa wa ugonjwa huo Wilayani Kishapu jana alipofika katika kituo hicho kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akionesha mfano wa namna bora ya kunawa wa Mikono kabla ya kuanza ukaguzi wa Kituo cha Afya Kishapu kitachotumika kuhudumia wagonjwa Corana kama atatokea mgonjwa wa ugonjwa huo Wilayani Kishapu jana alipofika katika kituo hicho kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara ndogo ndogo wa matunda na nyanya kando ya mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
…………………………………………………………………………………
Na Anthony Ishengoma- Sinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack amewataka wazazi na walezi mkoani Shinyanga kutowaruhusu watoto wadogo kwenda katika mikusanyiko hususani minada ya mazao na mifugo kama hatua muhimu ya kuwakinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wakati alipotembelea mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko katika Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwa lengo la kujionea utekelezaji wa agizo la serikali linalowataka wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa corona ikiwemo kuweka maji na sabuni katika maeneo yanayokutanisha watu wengi pamoja na kukaa umbali wa mita moja.
Bi. Tellack ameonya kuwa huu si wakati wazazi kutembea na watoto wao kutokana na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona na kuwataka kusubiri mpaka wakati ugonjwa huu utakapokuwa umedhibitiwa kwani uwezo wa watoto kujikinga ni mdogo sana.
Pamoja na agizo hilo la Mkuu wa Mkoa kwa wakazi na wafanyabiashara katika minada ya mifugo pia hakuridhishwa na hatua za zuinazochukuliwa na uongozi wa mnada huo za kuhakikisha wale wote wanaoingia mnadani hapo wanasafisha mikono yao baada ya kujionea mnada huo ukiwa na njia zaidi ya moja ya kuingia mnadani hapo na kutoa nafasi kwa baadhi ya watu kujipenyeza ndani ya eneo hilo bila kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona.
Bi. Tellack amewataka wafanyabiashara mnadani hapo kuhakikisha wanajikinga na maambukizi hayo kwa kila mmoja kunawa mikono yake kila mara na kuhakikisha wanakuwa na vitakasa mikono (sanitizers) kwa vile wanao uwezo wa kuvinunua kama hatua muhimu ya kujikinga na hatari ya maambukizi hayo.
‘’Nunueni vitakasa mikono kwa ajili ya usalama wenu kwa sababu hamuwezi kukosa fedha ya kununua ya kiasi cha shilingo elfu nne na miatano na hata kama ni shilingi elfu kumi kwa ajili ya kujikinga na kuwakinga wengine.’’Aliendelea kusema kiongozi huyo wa Mkoa.
Agizo kama hili pia lilitolewa na Mkuu wa Mkoa kwa wafanyabiashara ndogo wanaofika eneo la mnada kwa lengo la kujipatia kipato tofauti na mifugo inayouzwa mnadani kuhakikisha wanakuwa na maji na sabuni vinginevyo watozwe faini kwa kushindwa kutekeleza agizo hilo muhimu la Serikali.
Pamoja na kutembelea mnada huo Bi. Tellack pia alitembelea Kituo cha Afya cha Wilaya ya Kishapu kilichoandaliwa kama sehemu maalumu ya kupeleka wagonjwa wa corona endapo watabainika Wilayani humo kama hatua muhimu ya kujionea ni namnagani Wilaya ya Kishapu imejipanga kukabiliana na ugonjwa huo.
Akiwa katika kituo hicho cha Afya Mkuu wa Mkoa amejionea vifaa vnitakovyotumiwa na waudumu wa Afya kujikinga na kuwahudumia wagonjwa na kuwataka wahudumu hao kuwa tayari kwa lengo la kukabiliana na kuhudumia wagonjwa hao kwa tahadhari kubwa.
Mnada huo unaowakutanisha wafanyabiashara wa mifugo kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Shinyanga na mikoa jilani ufanyika kila Siku ya Alhamisi na kuvuta wafanyabiashara wa aina nyingine nje na ndani ya mnada huo ambao pia wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuweka vitakasa mikono katika maeneo yao ya biashara.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments