Marekani: Chui ‘Nadia’ akutwa na Virusi vya Corona, amuambukiza dada yake ‘Azul’ na Simba watatu kutoka Afrika | ZamotoHabari.



Chui wa kike wa Malaysia mwenye umri wa miaka minne katika bustani ya wanyama nchini marekani amepatikana na virusi vya corona.

Bustani hiyo ya Bronx katika mji wa New York, inasema kwamba matokeo hayo yalithibitishwa na maabara ya huduma ya afya ya mifugo mjini Iowa.

''Nadia, na dadake Azul pamoja na Chui wengine wawili na simba watano wa Afrika walianza kikohozi kikavu na wote wanatarajiwa kupona kabisa," ilisema taarifa ya uongozi wa bustani hiyo.


Chui hao wanaaminika kuambukizwa na mfanyakazi mmoja wa bustani hiyo.

''Tulimpima chui huyo kwa jina Nadia katika harakati za kuchukua tahadhari na tutahakikisha kwamba maarifa yoyote tutakayopata kuhusu Covid-19 tutayasambazia ulimwengu unaojaribu kuelewa ugonjwa huu'', ilisema bustani hiyo ya wanayama katika taarifa yake siku ya Jumapili.

Hamu ya kula ya Chui hao ilipungua lakini kwa sasa wanaendelea vyema chini ya uangalizi na madaktari wa wanyama.

Bustani hiyo imesema kwamba haijui virusi hivyo vitawaathiri vipi wanyama kama chui na simba kwa kuwa spishi tofauti zinaweza kuathirika tofauti kwa maambukizi mapya, lakini wanyama wote watawekwa chini ya uangalizi wa karibu.

Hata hivyo wanyama wengine wanne katika bustani hiyo ikiwemo Chui na duma hawajaonyesha dalili zozote za ugonjwa huo.

''Wanyama wetu waliathiriwa na mtu ambaye alikuwa akiwaangalia ambaye aliambukizwa virusi hivyo kabla ya kuanza kuonyesha dalili,'' ilisema bustani hiyo ya wanyama.

Chui wote waliokuwa na dalili walifungiwa katika eneo moja la bustani hiyo.

Bustani zote nne zinazosimamiwa na shirika la uhifadhi wa wanyama pori mjini New York , ikiwemo bustani ya Bronx wamefungiwa na hawawezi kuonekana na raia tangu tarehe 16 Mwezi Machi.

Mikakati mipya sasa itawekwa ili kuwalinda wanyama hao na wasimamizi wao katika bustani zote.

Hakuna ushahidi kwamba mtu yeyote ameambukizwa na Covid-19 na wanyama nchini Marekani, ikiwemo wanyama wanaofugwa nyumbani kama vile paka na mbwa, taarifa hiyo ya bustani ya Bronx ilisema.

Wataalamu wa uhifadhi wa wanyama pori wameonya kwamba virusi hivyo vinaweza kuwa tishio kwa wanyama pori kama vile sokwe - na wamesema kwamba mikakati inahitajika ili kupunguza hatari ya wanyama wengine kama vile gorilla chimp na urangutan.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini