Mzee Yusuph "Walinitenga..Wamesikia Narudi Mjini Wananipigia" | ZamotoHabari.



Aliyewahi kuwa muimbaji wa nyimbo za muziki wa Taarab Mzee Yusuph, amesema kuwa yeye alipotangaza kuachana rasmi na muziki huo, wasanii wenzake wengi walimtenga na hakuna hata ambaye alikuwa akimjulia hali, lakini baada ya kutoa kauli ya narudi mjini wengi wameanza kumjulia hali.

Hayo ameyabainisha wakati akizungumza kwenye kipindi cha DADAZ, kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

"Sikuwa karibu na mwanamuziki yeyote kwa sababu wote walinitenga na kunikataa, lakini baada ya kusema narudi mjini, wengi wamekuwa marafiki zangu, tunasalimiana meseji nyingi, simu yangu ilikuwa inakaa na chaji masaa 50, sasa hakuna, nikasema kweli shetani ni shetani tu na binadamu ni binadamu tu" amesema Mzee Yusuph.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini