Wazururaji Wote DAR Leo Kukiona Cha Mtema Kuni..Paul Makonda Atoa Onyo | ZamotoHabari.


Leo April 6, 2020, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ataanza rasmi zoezi la kuwakamata wazururaji wote wa Mkoa huo, wanaoingia mjini bila ya kuwa na kazi yoyote ikiwa ni tahadhari ya Virusi vya Corona.

Makonda amesema kuwa haina haja kwa mtu kuendelea kuzurura ili hali anatambua kabisa Dunia ipo kwenye wakati gani na hivyo mtu kama hana kitu cha msingi cha kufanya ni bora abaki nyumbani.

"Umuhimu wa kuchapa kazi uko palepale, kuanzia Jumatatu tutakamata wazururaji wote mjini wasiokuwa na kazi ya maana, hao ndiyo wanaosababisha mikusanyiko isiyokuwa na tija, unaenda stendi, Sokoni, Bandarini huna kazi huo ni uzururaji unahatarisha maisha ya watu wengine" amesema Makonda.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini