Watu 21 wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa kipindupindu kusini mashariki mwa Nigeria.
Mratibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ebonyi Dk. Eyo Nora ametangaza kwa waandishi wa habari kuwa watu 21 wamekufa katika janga la kipindupindu la nchini humo.
Nora amebaini kuwa kesi 155 za kipindupindu zimegunduliwa katika jimbo hilo, na kwamba dawa za dharura na vifaa vya matibabu vimepelekwa katika sehemu husika.
Nora amesema kuwa wameanza kuchukua hatua za kuzuia mlipuko huo, unaosababishwa na ukosefu wa maji safi na usafi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments