Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, amesema kuwa Serikali inawafuatilia watu wote wanaoendelea kutoa taarifa za upotoshaji kuhusu vifo vinavyotokea mkoani humo, hususani kifo cha Abate Mstaafu Alcuin Nyirenda wa Abasia ya Hanga, kilichohusishwa na ugonjwa wa Corona.
RC Mndeme amesema kuwa bado watahakikisha wale wote wanaopotosha kifo cha Abate Nyirenda wamekamatwa.
"Tunaendelea kuwafuatilia wale wote wanaoendelea kutoa taarifa za upotoshaji kwa kutumia mitandao ya kijamii na sehemu zingine, kwa kusema fulani amekufa kwa Virusi vya Corona" amesema RC Mndeme.
Abate Mstaafu Alcuin Nyirenda amefariki Dunia Aprili 4, 2020, katika hospitali ya Peramiho alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya uzee na alizikwa Aprili 8 wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments