"Sitaki Mtu Kumsalimia Mwanaume Wangu" - Lulu Diva | ZamotoHabari.


Mrembo kutoka kwenye kiwanda cha BongoFleva Lulu Diva, amesema endapo ataanza kuwa kwenye mahusiano hataki na hatamani rafiki yake yeyote, amshike mkono au kumsalimia mwanaume wake.


Lulu Diva amesema kwa sasa yupo "single" ila anaogopa kuwa na mahusiano kwa sababu marafiki zake wakijua itakuwa shida, ndiyo maana huwa anapendelea mahusiano ya siri.

"Mimi naogopa kuwa kwenye mahusiano ambayo marafiki zangu watajua, na nitakapokuwa nimeanza mahusiano sitamani hata rafiki yangu amshike mkono au amsalimie mwanaume wangu, maana siku hizi watu wamekaa kuangalia mahusiano ya watu kama wamegombana au wataachana lini, hawataki heri wanapenda matatizo tu" ameeleza Lulu Diva.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini