Wazazi Wawapa Watoto wao Majina ya Corona na Covid | ZamotoHabari.


Wazazi kutoka Raimpur katika Mji wa Chhattisgarh nchini India, wameamua kuwapa watoto wao ambao ni mapacha wakiume na wakike, majina ya Corona na Covid, kutokana na dunia nzima kuwa katika janga la ugongwa wa Virusi vya Corona.


Wazazi wakiwa na watoto wao mapacha ambao wamewapa majina ya Corona na Covid

Watoto hao ambao wamezaliwa usiku wa kuamkia Machi 27 mwaka 2020, katika hospitali ya Serikali ya Ambedkar inayopatikana huko Raimpur.

Mama wa watoto aitwaye Preeti Verma mwenye miaka 27, amesema sababu ya kuwapa majina hayo ni kutokana na ugumu ambao dunia inakutana nayo kuhusu janga la Corona, pia wametaka kuweka kumbukumbu ya historia kupitia majina hayo.

"Tumebarikiwa kupata watoto wawili mapacha, wa kiume anaitwa Covid na wakike ni Corona, tumewapata hawa kutokana na ugumu ambao tunakutana nao kwahiyo mimi na mume wangu, tumeamua kuwapa majina haya kwa sababu ya kumbukumbu tunajua virusi hivi ni hatari na vinatishia maisha ya watu" amesema mama wa watoto hao.

Nchi ya India inakadiriwa kuwa na watu Bilioni 1.4, hadi sasa kuna kesi za ugonjwa wa Corona zipatazo 2567, na idadi ya waliofariki ni 72.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini