Yafahamu Makosa Wanayofanya Wanawake Wengi Kwenye Safari ya Uchumba na Kuishia Kutafunwa na Kutemwa Kama Kapi la Mua | ZamotoHabari.




Kitu ambacho wasichana wengi hukosea ni pale wanapogeuza uchumba au uhusiano wa kawaida kuwa ndoa. Si busara kumpa mwanaume kila kitu katika mahusiano ya uchumba wakati hujaoana naye. Unamfulia nguo, unalala kwake, unampikia chakula wakati yeye ni boyfriend tu!

Shida inakuja pale ambapo mwanaume anajiuliza ni kwanini aingie gharama za kukuoa ikiwa umeshakuwa mke bila hata kukutolea mahari wala kukuvisha pete kwenye kidole? Kwanini akuoe wakati tayari ameshajua kila kitu kuhusu wewe? Kwanini anunue ng’ombe kama maziwa na nyama vyote anapata bure?

Kumbuka wazazi wetu walikuwa makini sana na hayo na mwanamke yeyote enzi hizo hakujifanya mke wakati ni mchumba tu. Uchumba ni daraja tu la kupita kufikia ndoa. Huwezi kugawa zawadi zote ambazo zipo kwenye begi kabla ya kufika kwa mwenyeji wako katika safari ya kuelekea kwenye ndoa

Wanaume ni binadamu si Mungu na kila binadamu ana sifa ya kugeuka nyuma pale anapoona njia anayoenda si yenyewe.
Uwe na lengo la kuhakikisha unaweza kuweka mipaka katika uhusiano wako na usimfanye huyo mwanaume ndio kila kitu hapa duniani kwani kuna siku anaweza kubadili uamuzi ndipo kujuta kutakuja.
Ni busara kwa wewe msichana hata kama una mchumba wako na mnapenda sana, asikufanye usahau malengo yako katika maisha yako, asikufanye usahau kama unatakiwa kuwa msaada kwenye familia yako. 

Usijiachie kupita kiasi endelea kujihusisha na kazi yako, taaluma yako kiasi kwamba hata ikitokea amekuacha huwezi kuchanganyikiwa kwa kupoteza vitu vyako muhimu katika maisha yako.

Kama umewekeza kwa mchumba upendo na mapenzi ya asilimia 100 Je, baada ya kuoana utawekeza kiaasi gaini? Usijifanye mke wakati wewe ni girlfriend au mchumba tu



  


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini