Yanga Yatuma Ujumbe Mzito Simba Kisa Tshishimbi "Mtasubiri Sana" | ZamotoHabari.



WANAFAMILIA wa Yanga ambao ni mabosi pia Kampuni ya GSM imesema kuwa iwapo kuna klabu ndani ya Bongo ama nje ya nchi itahitaji saini ya nahodha Papy Tshishimbi inapaswa isubiri mpaka mkataba umalizike.

Maneno hayo ni ujumbe kwa watani wao Simba ambao ilielezwa kuwa wanahitaji saini ya nyota huyo ili akaongeze makali ndani ya kikosi cha Simba.

Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya GSM Injinia Hersi Said amesema:"Kuhusu kapteni Tshishimbi yeye ni mchezaji muhimu na tumemalizana naye ambapo dili limekamilika na yeye mwenyewe amekubali kwa kusema 'dealdone'.

"Kwa wale ambao wanahitaji kuipata saini yake basi inawabidi wasubiri mpaka pale mkataba utakapoisha ili waweze kuipata saini yake ila kwa sasa atabaki ndani ya Yanga,".

Inaelezwa kuwa mkataba wa Tshishimbi ambao ulikuwa unameguka mwezi wa nane umeboreshwa kwenye upande wa maslahi jambo ambalo limemfanya akubali kusaini.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini