Donald Trump Kama Magufuli...Aagiza Magavana Kufungua Sehemu za Ibada Marekani.. | ZamotoHabari.


Rais wa Marekani, Donald Trump amewataka Magavana nchini humo kufungua makanisa, misikiti na masinagogi, kwa kusema ni huduma muhimu.

Akitoa agizo hilo amewataka Magavana kuchukua uamuzi sahihi na kuruhusu sehemu za ibada kufunguliwa mara moja kwani Marekani inahitaji maombi zaidi.

Amesema baadhi ya Magavana wamefungua maduka ya vilevi na kliniki za kutoa mimba lakini wameacha sehemu za ibada, jambo ambalo amedai sio sahihi hivyo anasahihisha kosa hilo kwa kufanya ibada kuwa huduma muhimu.

Hata hivyo, kauli yake imeacha sintofahamu kwakuwa Serikali haina mamlaka ya kikatiba kuamuru majimbo binafsi kufungua biashara, makanisa au Shule.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini