ASKOFU na Mchungaji kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema kuwa amewachukia viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mara baada ya viongozi hao kuwatukana na kuwakashifu watumishi wa Mungu.
Gwajima aliyasema hayo leo Jumapili, Mei 17, 2020 wakati alipokuwa anahojiwa na kipindi cha Soul Food kinachorushwa kila Jumapili kupitia spika za +255 Global Radio. Gwajima alifunguka kuwa alilkuwa shabiki mkubwa wa Chadema lakini alikuja kuwachukua kutokana na maneno yao yasiyofaa kwa watumishi wa Mungu.
“Mimi nilikuwa ‘fan’ wa Chadema, lakini walikuja kuniudhi baada ya kuanza kuwatukana watumishi wa Mungu. Historia ya dunia inasema, hakuna aliyewahi kumtukana mtumishi wa Mungu na akabaki sawa hata kama halijifanya kuwa sawa, ‘just matter of time’.
“Unakumbuka mara tu ya uchaguzi kuisha, Mheshimiwa Rais akawa anazindua ule mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa ‘Stiegler’s gorge’, akakaribisha watumishi wa Mungu wote. Tulikuwa watumishi wengi, askofu Kakobe, Askofu Gamanywa, Askofu Mwingila.
“Kumbuka umeme siyo ishu ya siasa, ni ishu ya watu wote, tulipotoka pale viongozi wa Chadema wakaanza kutukana, wakasema hawa watumishi wa Mungu ni wasaka tonge, wenzangu wakapaniki, mimi nikasema natulia maana mimi risasi zangu ni za kuulia Tembo, nikawaambia wenzangu tulieni kwanza.
“Ikaja tena hii ishu ya Covid-19, Rais Magufuli, akatoa tamko kuwa tuombe, wao wakawa wanabeza tena maombi yetu, wakisema ni maombi gani hayo. Hiyo haijaisha tena Rais akatoa tamko kuwa makanisa yasifungwe, wao wakaanza kusisitiza makanisa yafungwe watu wasalie nyumbani.
“Mimi nikashangaa kwa mara ya kwanza, hakuna mtu ambaye atasema kuwa makanisa yafungwe, akitokea mtu kama huyo asili yake ni shetani, nikashangaa nikasema hawa jamaa zangu wamepatwa na nini.
“Ndipo nikasema hawa jamaa wanataka viboko, bado sijapiga vizuri nawasikilizia, maana naona kuna mtu mwingine anakimbelembele, namsikilizia maana mimi risasi zangu ni za moto siyo za kupigapiga hovyo,” alifunguka Gwajima.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments