Wimbo wa dhahabu ya Dully Sykes ulifanya vizuri sana miaka 12 iliyopita, ambapo aliwashirikisha Mr Blue na Joslin bila ya wao kujijua kwa sababu kipindi hicho wawili hao walikuwa na bifu na kushindanishwa.
Sasa Dully Sykes ametueleza historia ya wimbo huo kwa kusema alikuwa hana mpango wa kumshirikisha Joslin, pia aliingia studio na wanawake wawili kisha kuipa mgongo mike wakati anarekodi.
"Ngoma ilikuwa ni kumshirikisha Mr Blue peke yake lakini siku ambayo mimi narekodi Joslin alikuwepo studio , kipindi hicho hakukuwa na mahusiano mazuri kati Mr Blue na Joslin nikaona hii idea inaweza ikaleta nguvu kwenye ngoma yangu, hata wakati wakuingiza verse kila mtu aliingiza kivyake bila ya wao kuwaambia na kwenye ushindani walikuwa wanashindanishwa wao tu".
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments