Mchezaji Gwiji wa Zamani wa Yanga Afariki Dunia... | ZamotoHabari.



Aliyewahi kuwa mchezaji na Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Lawrence Mwalusako amefariki dunia leo Asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.



Taarifa hiyo imethibitishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Tanzania, Mussa Kisoki ambapo amesema kuwa Mwalusako alikuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji.

Katika maisha yake ya soka, Lawrence Mwalusako aliazia katika klabu ya Waziri Mkuu ya Dodoma kisha akajiunga na Yanga ambapo baada ya kustaafu alikuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo.

Mussa Kisoki amemzungumzia Mwalusako kuwa ni mtu mcheshi tangu alipokuwa mchezaji na hata katika uongozi wake, pia alisifika kwa kusimamia kwa umakini mipango mbalimbali, akitaja mfano kuwa alikuwa hana masihara hata katika masuala ya mazoezi ya klabu.

Taratibu za kuchukua mwili zinaendelea na msiba huo utakuwepo Ubungo Jijini Dar es Salaam, ambapo kwa mujibu wa Kisoki, familia itatoa taarifa rasmi baada ya taratibu zote kukamilika.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini