Kwa Ubunifu Huu Platnumz Ataendelea Kutamba kwa Miaka Kadhaa ijayo | ZamotoHabari.


Licha ya kutaka tu mziki mzuri lakini tunapenda vionjo vingine pia kutoka kwa Mwanamuziki. Msanii/Mwanamuziki/Mburudishaji yafaa kuishi kisanii kama kazi uliyochagua inavyokutaka na si kuleta mambo ya faragha au kujifanya mwenye staha saana (mradi usivunje sheria).

*Fashion, namna anavyovaa.
*Mwonekano, Asikwambie mtu mwonekano hasa body unasaidia sana kuigusa hadhira.
*Kujithaminisha, jifanye ghali sio wa rahisirahisi.
*Dance/Cheza, Hili hadhira inafurahishwa nalo sana!
*Life style ya kisanii.
*Mbinu kali katika kutafuta na kuyaona masoko ya muziki/bidhaa yako.

Jamaa ni msanii aliyekamilika kwa ninavyomtazama, anajua sana kizazi hiki kinataka nini kutoka kwa msanii/mburudishaji na anatupatia kwa kweli.

Hili limefanya karibu Media zote hasa hizi Online kujikuta zinahitaji mno habari za Diamond ili kujitengenezea wafuatiliaji wa media zao.

Yaani kwa sasa media isiyoandika au kuzungumzia Diamond na WCB kwa ujumla inajichelewesha yenyewe!!

Tukubali au tukatae lakini Diamond anabaki kuwa ndie alama au dira kwa upande wa burudani hasa ya kizazi kipya hapa Tanzania. Ni vile tu Sisi weusi tumeumbwa kuchukia wanaofanikiwa kuliko kujifunza kupitia kwao!

Big up Platnumz.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini