Nguvu ya Mitandao ya Kijamii: Posti za Miaka 6 iliyopita Zamnyang'anya Followers, Zamkwamisha Kushiriki Miss South Africa 2020 | ZamotoHabari.



Mwanadada Bianca Schoombee wa Afrika Kusini amejitoa katika kinyang’anyiro cha mashindano ya Miss South Africa kwa mwaka 2020. Taarifa hiyo imetolewa na wakala wake.

Bianca alipata mapokezi makubwa katika mtandao wa Twitter baada ya kuposti picha zake kama sehemu ya ushiriki wake katika mashindano hayo.

Inaelezwa kuwa katika maombi ya kushiriki mashindano hayo yaliyofunguliwa mnamo Mei 11, nyota ya Bianca ilianza kung’aa na hivyo kutabiriwa kuwa mrembo ambaye angepokea taji la Miss South Africa baada ya Sasha-Lee Olivier ambaye analishikilia kwa sasa.

Hata hivyo, upendo toka kwa mashabiki wake ulibadilika ghafla na kuwa hasira kali baada ya posti zake za miaka 6 iliyopita zilizoashiria ubaguzi wa rangi na matusi ya waziwazi kufukuliwa na kusambazwa mitandaoni.

Akaunti yake ya Twitter ilipokea pigo kubwa ambapo hadi siku ya Jumatano, mashabiki wanaomfuatilia walipungua na kufikia 700 kutoka wafuasi 8,000 siku chache kabla.

Mlimbwende huyo aliomba radhi kupitia Twitter akisisitiza kuwa alitenda hayo akiwa bado binti mdogo wa miaka 14 na kwamba amebadilika lakini watumiaji wa mitandao hawakuelewa hilo

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini