Baraza la Sanaa Taifa BASATA limetoa mwongozo kwa wasanii, watayarishaji wa matamasha na wamiliki wa maeneo ya burudani kuhakikisha wanazingatia miongozo yote iliyotolewa na Wizara ya Afya kuelekea tarehe 29 Juni mwaka huu ambapo shughuli zote zilizokuwa zimesimama kufuatia janga la Corona zitakuwa zinarejea kama alivyoelekeza Rais Magufuli.
Itakumbukwa, Rais Magufuli alitoa tamko hilo Juni 16, wakati akihutubia bunge la 11 jijini Dodoma na kuruhusu shughuli zingine zote ziendelee nchini ikiwemo sherehe mbalimbali kama harusi na mikusanyiko mingine.
Aidha, katika mwongozo uliotolewa na #BASATA, limesisitiza suala la elimu kwa jamii wakati wote ambapo shughuli yoyote ya kiburudani itakua inaendelea.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments