Akon Alikataa Kumsaini DRAKE Kwenye Lebo yake ya Muziki Kisa Alikuwa Hajui Kuimba | ZamotoHabari.



Drake ndiye msanii wa kizazi hiki ambaye amevunja na kuweka rekodi kibao za muziki ambazo wengi walikuwa wakiziota.

Ambacho unatakiwa kufahamu ni kwamba AKON alikataa kumsaini Drake kwenye label yake ya muziki maarufu KONVICT Music, kwa kile alichowahi kukieleza kwamba [Drake] hakuwa mkali wakati anasikilizishwa nyimbo zake.

Kwenye moja ya mazungumzo yake mwaka 2015, Akon alisema kwamba Kardinal Offishall alimletea baadhi ya nyimbo za Drake, lakini hakuvutiwa nazo na kushindwa kumsaini. Hii ilikuwa kabla ya Drake hajaachia dundo lake la muda wote "Best I Ever Had" la mwaka 2009.

"Kiukweli nilimpita na kushindwa kumsaini kwa wakati ule, hakuwa anasikika (sound) kama anavyosikika sasa hivi. Zilikuwa ni nyakati ambazo alikuwa anajitafuta."alieleza Akon ambaye label yake imewainua wengi kimuziki akiwemo; Lady Gaga, T Pain, French Montana na wengine kibao.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini