WASANII nguli wa Bongo Fleva, Alikiba na Diamond Platnumz, ni miongoni mwa wasanii walioalikwa na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao unafanyika leo, Jumamosi, Julai 11, 2020, jijini Dodoma.
Diamond ameongozana na wasanii wake wa Lebo ya Wasafi (WCB) akiwemo Rayvanny, Mbosso, Zuchu Queen Darleen, Lavalava, dansa wake Mose Iyobo, mameneja wake, Mkubwa Fella, Babu Tale na Sallam SK.
Aidha, ameonekana katika picha akiwa na Bilnas na Marioo wakiwa Dodoma katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM.
Mbali na wasanii hao, wengine ni Msanii wa Mashairi, Mrisho Mpoto na wengine kibao wakiwemo wa Bongo Movies akiwemo Dude na tasnia nyingine.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments