MZAZI mwenziye Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ametoa kauli inayoashiria moja kwa moja, ana kiu ya kumpata mtu sahihi kwenye maisha yake.
Kupitia mtandao wa nchini Uganda, Zari ameweka wazi kuwa, ana miezi saba sasa hamjui mwanaume tangu aachane na aliyekuwa mume wake, King Bae.
UNAMKUMBUKA KING BAE?
King Bae ni yule mwanaume ambaye alidaiwa kumuoa katikati ya mwaka jana na ndoa yao kuwa gumzo mitandaoni, huku gumzo zaidi likiwa ni kwa nini Zari hamuoneshi sura mwanaume huyo.
AMCHANA…
Zari amesema, mwanaume huyo hakuwa na malengo na yeye bali alikuwa ni mtu wa kumtumia na kama hiyo haitoshi, alikuwa mtu wa kuigiza maisha ambayo si ya uhalisia.
“Kama mnavyojua mimi najituma, nafanya kazi na ninaweza kujitegemea mwenyewe, lakini yule alitaka kuniigizia maisha,” alisema Zari.
WATU KIBAO WANAJIPITISHA
Mama huyo wa watoto watano, alisema kwa sasa anapokea maombi mengi kutoka kwa wanaume tofauti lakini anakuwa muangalifu, kwani yeye ana mapenzi ya dhati na akipenda anapenda kweli.
“Mimi nikipenda napenda kweli, hivyo sipo tayari kuumizwa tena, lazima niwe makini,” alisema Zari.
KING ALIKUWA MUONGO
Akimzungumzia zaidi King Bae, Zari alisema, jamaa huyo alikuwa akikodisha magari ili kujionesha kwamba yupo vizuri kimaisha wakati hayo magari hayakuwa yake.
“Alikuwa anakodi magari ya gharama kama Ferari, Rolls Royce na Maserati lakini hata hivyo aliishia kuaibika maana alikuja kudaiwa na kushindwa kuyalipia.
“Hata nyumba ambayo alikuwa amepanga, alishindwa kulipia na kujikuta akifukuzwa kwa kushindwa kulipa kodi. Huo ndiyo ulikuwa mwisho wangu na King Bae,” alisema Zari.
Zari alisema, mapenzi sio kitu kigumu, lakini tatizo ni pale unapokutana na mtu ambaye si sahihi kama ilivyomtokea yeye.
MAISHA YA SASA
Akizungumzia maisha yake ya sasa, alisema anakuwa makini zaidi na wanaume kwani licha ya kwamba amekuwa staa kwa kipindi cha takriban miaka 20, lakini haoni sababu ya wanaye kuona anabadilibadili wanaume.
“Ninachokifanya kwa sasa, namuweka tu mwanaume karibu lakini hatuwi wapenzi. Yeye anaweza jua nampenda kumbe mimi sipo hapo,” alisema Zari.
KUHUSU DIAMOND…
Alipoulizwa kuhusu kurejesha majeshi kwa mzazi mwenzake Diamond au Mondi, Zari alisema kwa sasa wao wanalea watoto wao tu.
“Diamond na mimi tunalea tu watoto hakuna kingine,” alisema.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments