Diamond Platnumz Arudishwa kwa Tanasha Dona | ZamotoHabari.


MWONEKANO mpya wa mzazi mwenza wa na mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna umewatoa wengi udenda huku baadhi wakimtaka jamaa huyo kurejesha majeshi.

Wikiendi iliyopita Tanasha aliposti picha zake mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram ukimuonesha amenona kwelikweli ndipo yakaibuka maneno kibao kwamba Diamond au Mondi ajitafakari kisha arejee kwa Tanasha.

Tanasha aliposti picha akiwa amekaa kwenye gari na kuandika; “How cute with this old school car on to other things.’’

Baada ya picha zake kumuonesha amekuwa mcharo ndipo wananzengo wakaanza kusema kuwa Mondi alikuwa akimtesa ndiyo maana alikonda na kufupaa, lakini sasa mtoto anaita.

“Unaona sasa dada wa watu kapendeza, kule alikuwa akiteswa tu na kupewa stresi kila siku ndiyo sababu alikondeana,’’ aliandika mmoja wa wafuasi.

Mbali na mashabiki zake pia baadhi ya mastaa kama Nandy walionekana kuuelewa muonekano huo wa Tanasha kwani waliweka maoni kwenye posti hiyo wakimsifia.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini