Wakuu, mi nauliza tu!
Hawa ni mastaa wetu, ‘vioo’ vya jamii. Basi wengi wao hupenda ku-name akaunti zao ‘official’.
Yaani kila msanii ana prefix- au suffix- official, hata wale uchwara atajiita ‘officialuchwara’ au ‘utopoloofficial’.
Napata tabu huenda mimi sielewi, na wala siioni huko kwa mabeberu tunakojifunza. Wajuvi nijuzeni, nami nipate kujua.
Nini maana ya kuwa ‘official’ kwenye hizi kurasa zetu?
Asanteni.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments