Kwenye maisha kila mtu kajiwekea principles zake na utaratibu wa Maisha.. Ni sahihi sana lakini Kuna vingine vinahitaji Utashi wa kibinadamu kung'amua Hasara na Faida zake..
Kuna watu wamejiwekea utaratibu kwamba Hata iweje, Basi Namba ngeni itapiga sana na kamwe hatopokea.. Sijui ni madeni au basi tu hataki lakini ndo alivyoniwekea.. Hii iko pande zote kwa Baadhi ya wanaume na Wanawake.. Wanawake wengi wanasema wao huepuka Usumbufu kwani mara nyingi huwa ni wanaume wakware wanaotaka penzi lao.
Dhana hii kwa upande mmoja ni sahihi.. Lakini Je, huoni haja ya kumsikia anayekupigia ni nani kabla huja ignore? Na unakuta wewe ni mfanyabishara, mfanyakazi na pengine Mtafutaji wa kazi ume apply huko na huko.. Sasa umepigiwa simu ya interview na hupokei unataka uje kumlaum nani?
Juzi Mtu wangu wa karibu Kapigiwa sana simu Kwa namba mpya na hakuipokea maksudi kabisa zaidi ya mara nne.. Huku akibetua mdomo "Wanaume bana huyu nae anataka kunisumbua tu" Lakini baadae kupitia Namba hyo hiyo akatumiwa Msg Kwamba Kaka yake kafariki kwa Ajali.. Ndo akaanza kutoa vilio kama punda mwenye Njaa!
Wakati mwingine tuangalie misimamo yetu kama ina tija kwenye Maisha.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments