Kimenuka..Marekani Yaufunga Ubalozi Wake Mdogo Nchini China | ZamotoHabari.


Huku zikiwa zimesalia saa kadhaa kabla ya kufikia Jumatatu asubuhi ambao ndio muda wa mwisho kwa wafanyakazi wa ubalozi huo wanaonekana wakibeba maboksi ya makablasha yao na mifuko ya takataka.

Wakati huo huo, umati wa wakazi wa eneo hilo umekusanyika nje ya ubalozi huo, ukiwa umebeba bendera za China na kupiga picha.

China ilichukua hatua ya kufunga ubalozi huo kujibu hatua ya Marekani kuufunga ubalozi wake mdogo wa Houston, Texas, wiki iliyopita.

Baada ya muda wa mwisho uliowekwa wa saa 72 kwa wanadiplomasia wa Uchina kuwa wameondoka Houston kumalizika Ijumaa, taarifa zinasema wanaume walionekana kuwa ni maafisa wa Marekani walifungua kwa nguvu mlango ili kuingia ndani ya ubalozi huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema kuwa serikali ya Marekani mjini Washington iliamua kuchukua hatua hiyo kwasababu Beijing ilikua ''inaiba'' akili miliki.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uchina Wang Wenbin alijibu akisema hatua ya Marekani "mkanganyiko wa uongo wa chuki dhidi ya Uchina".

Vyombo vya habari vya taifa la China vimekua vikionesha picha za malori yakiondoka katika ubalozi mdogo wa Marekani, na wafanyakazi wa ubalozi huo wakiondoa vitu kutoka kwenye jengo la ubalozi.

Makumi kadhaa ya polisi wa China wamekuwa wakipelekwa nje ya ubalozi huo, wakiwataka watu waliokusanyika nje kushuhudia kinachoendelea kuondoka na kujaribu kuzuia vitendo vya uchokozi .

Hatahivyo, sauti zilizikika za watu waliokua wakizomea wakati basi likiondoka nje ya jengo hilo siku ya Jumapili, zimeeleza taarifa za shirika la habari la AFP.

Wakati wanadiplomasia wa China walipoondoka kwenye ubalozi wao Bouston kwa mara ya mwisho walizomewa na waandamanaji.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini