Janeth Raphael, Michuzi Tv
LICHA ya mara kadhaa kusema kwamba hatoweza kugombea nafasi za kisiasa kwa sababu nafasi yake ya utumishi wa kiroho ni kubwa, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametangaza kugombea Ubunge Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam.
Gwajima ametangaza nia yake hiyo ya Ubunge baada ya kuchukua fomu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Julai 14 ambapo alisindikizwa na familia yake.
Mara baada ya kutoka katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi kuchukua fomu, Gwajima aligoma kuzungumza kwa kirefu na wandishi wa habari na kuishia kutamka maneno machache tu "Itoshe kusema kuwa nimechukua fomu".
Katika moja ya mahubiri kanisani kwake siku za nyuma, Gwajima aliwahi kusema nafasi aliyonayo ya kuwaongoza waumini wake kiroho ni kubwa kulinganisha na nafasi za kisiasa duniani hivyo hana mpango wowote wa kugombea kama ambavyo ilikua ikizuka.
" Utumishi wa Mungu ni kila kitu, ni zaidi ya Rais wa Nchi, ni zaidi ya Uwaziri, ni zaidi ya Ubunge, sasa mimi kama Mtumishi wa Mungu siwezi kujishusha chini kwa kugombea hizo nafasi," Aliwahi kusema Gwajima kwenye moja ya mahubiri yake.
Gwajima atakabiliana na upinzani mkubwa kutoka kwa Halima Mdee was Chadema aliyeshikilia Jimbo hilo kwa mda mrefu na hapo Jana chama chake Cha Chadema kimempitisha tena kugombea Jimbo hilo.
Gwajima atakabiliana na upinzani mkubwa kutoka kwa Halima Mdee was Chadema aliyeshikilia Jimbo hilo kwa mda mrefu na hapo Jana chama chake Cha Chadema kimempitisha tena kugombea Jimbo hilo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments