WANAWAKE WAASWA KUTOKUKAA KIMYA UNAPOTOKEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA | ZamotoHabari.

 Msimamizi wa Miradi wa shirika linalosimamia haki za watoto (Bright jamii initiative), Godwin Mongi akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akifafanua mambo mbalimbali ya ukatili wa kijinsia kwa binadamu hasa watoto na wanawake. 

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TAFSIRI mbaya za Mila, desturi na mafundisho ya dini yatawa kuwa chanzo cha unyanyasaji, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na ukatili wa kijinsia.

Hayo yamesemwa na Msimamizi wa Miradi wa shirika lisilo la kiserikali linalosimamia haki za watoto (Bright jamii initiative), Godwin Mongi, akizungumza na michuzi blog jijini Dar es Salaam leo,  amesema kuwa ukatili unaotokea katika jamii ni matokeo na si chanzo au mizizi ya ukatili huo.

Mongi amesema kuwa licha ya kuwepo na matukio mengi ya unyanyasaji pamoja na ukatili katika jamii zetu lakini kumekuwepo na usiri mkubwa kati ya mtendewa wa ukatili huo.

"Lazima kila mmoja aonapo unyanyasaji wa kijinsia na ukatili popote alipo lazima atoe taarifa kwa vyombo vya kutetea na kutokomeza ukatili katika jamii."

"Unatendewa, anatendewa mtu lazima kutoa taarifa hiyo ili kila mmoja aishi salama mahali halipo......"Amesema Mongi.

Hata hivyo mongi amesema kuwa sheria za kutetea haki za wanawake na watoto katika jamii zipo wazi lakini zinashindwa kufanikiwa kwa ufasaha ni kutokana na kutokutoa taarifa kwenye vyombo husika.

"Sheria zipo wazi kabisa zinakataza na adhabu zake zipo wazi kinachofanya sheria ishindwe kuchukua mkondo wake ni mila na destuli pamoja na mafundisho mbalimbali yanayopotosha jamii  na kusababisha ukandamizaji kwa wanawake ambao ndio waathirika wenyewe. "

Licha ya hivyo amesema kuwa licha ya mwanamke kupata ujasiri wakwenda kuripoti katika kituo cha polisi bado anakuwa na fikra za kuwa ndugu zake watamwonaje na jamii itamchukuliaje.

Mongi ametoa mfano wa Zena Mohammed (Shilole) ambaye amevuka hatua na kufunguka kuhusiana na kitendo alichofanyiwa.

"Kitu alichokifanya Shilole ni matokeo tuu licha ya kuwa hatua aliyoipiga kufunguka (kusema) hii ni hatua kubwa aliyoifanya bila kuogopa na kutokufikili jamii itamchukuliaje!."

Wanaofanyiwa ukatili wakichukua hatua kama hii basi ukatili utapungua katika jamii zetu zote. Wanawake waache kukaa kimya kwa vitendo vya kikatili vinavyowatokea." Amesema Mongi.

Licha ya wanawake na watoto kuwa ni watu walio katika kundi maalumu lakini ndio wahanga zaidi katika ukatili wa kijinsia, pia kwa kiasi kikubwa ndio wanaopata unyanyasaji wa kinsia.

Hivyo wanawake kwa pamoja lazima kila mmoja achukue hatua ya kusema na kuvumua unyanyasaji unapotokea katika familia na jamii kwa ujumla.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini