Wataalamu wa mambo wanasema Master J na Shaa ni miongoni mwa Wachumba waliokaa kwenye uchumba kwa miaka mingi zaidi, pamoja na hayo kuna good news mwaka huu na ameisema Master J mwenyewe.
Producer huyo Mkongwe wa Bongofleva ameyasema haya “Naomba niseme ukweli, mwaka huu naoa kwa sababu tayari Mahakamani nimeshamaliza maswala ya mkataba kuvunja ile ndoa yangu ya kwanza kwahiyo Mwaka huu Mungu akijalia nafanya kweli”
“Hatimaye……….. na namshukuru sana Shaa kwa kunivumilia muda wote huu karibu miaka 15….. hata Isidingo si imeshaisha… hahahhhhhahahaaha, samahani sana na pole sana Mpenzi wangu” amesema Master J
Mara ya kwanza wawili hawa kukutana ilikua ni wakati Shaa alipokwenda Studio kwa MJ kurekodi wimbo wao wa kundi uitwao ‘hoi’ hiyo ndio ilikua mara ya kwanza kukutana nae kisha wakaenda South Africa kumalizia kurekodi,
“Tukaanza kuzoeana na kuwa karibu sababu tulikua tuko pamoja muda mwingi tukifanya kazi kila siku” amemalizia Master J.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments