Msanii wa filamu Bongo Niva Super Marioo ametuma salamu 3 kwenda kwa wapenzi wake wa zamani kwa kusema, wamkome kwa sababu amepata mpenzi mpya wa kizungu anayeishi nchini Uswizi.
Niva Super Marioo amesema yeye ndiyo msanii pekee wa Tanzania anayemtumia pesa mpenzi wake nje ya nchi kwa ajili ya ishu za masomo, ambapo ametoa onyo kwa ex zake.
"Mimi ndiyo Mtanzania wa kwanza kwa wasanii anayetuma pesa kwenda mbele kila baada ya mwezi ili mke apate matumizi kidogo, wengi wao wanasubiri pesa itumwe kule kuja huku, ninachowaambia ma-ex zangu sasa hivi nina pesa za kutosha, nina familia yangu muache kutuma meseji zenu za njaa, salamu zangu za mwisho mnikome maana nina mpenzi wangu yupo Uswisi halafu msomi, muelewa na ana akili kubwa" amesema Niva Super Marioo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments